STAA wa filamu Bongo,
Aunt Ezekiel na shostito wake Nice Chande, juzikati walijikuta
walitifuana kwa matusi makali ya nguoni nyumbani kwa rafiki yao Wema
Sepetu ‘Madam’ anayeishi mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es
Salaam.Chanzo makini cha habari kilichokuwa nyumbani kwa Wema,
kililidokeza gazeti hili kuwa waigizaji hao wakiwa na rafiki yao
mwingine, walianza kutukanana kwa jambo ambalo halikuweza kubainika mara
moja, huku Madam akijitahidi kuwasuluhisha bila mafanikio.
Wakiwa
na dalili zote za kubugia kiburudisho cha kutosha kilichowafanya
wasione vibaya kupaza sauti za matusi mbele za watu, marafiki hao
walitoka ndani ya nyumba hiyo na kuendelea kutukanana kana kwamba hawana
akili nzuri.
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akipozi.
Baada
ya kuona watu wameanza kukusanyika usiku huo ili kushuhudia sinema
hiyo, Aunt, Nice na rafiki yao walijipakiza kwenye gari, huku Aunt akiwa
nyuma ya usukani na kuanza safari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwake,
Mwananyamala, lakini safari yao iliishia hatua chache mbele baada ya
dereva huyo kulitumbukiza mtaroni gari hilo.
Kuona
hivyo, watatu hao walishuka na kuanza kurudi tena nyumbani kwa Wema,
ambaye aliendelea kuwasihi lakini wakiendelea kushambulia kwa maneno
makali, kila mmoja akimlaumu mwenzake kuwa ndiye chanzo cha ajali ile.
Kwa pamoja kutoka kulia Aunt Ezekiel, wema na Nice wakila ujana.
Nyumbani
kwa Wema, wasanii hao walimuomba msaidizi wake, Petit Man aende
kuwasaidia kulinasua gari hilo mtaroni, kazi ambayo ilifanywa na vijana
wa mtaani hapo waliolipwa kiasi cha shilingi 50,000
No comments:
Post a Comment