“Mimi
nimefanya hivi kwa kupenda kwangu, sijalazimishwa na mtu. Nimejisikia
kufanya hivi kwa sababu nampenda sana Shilole…tukiachana basi lakini
mimi nitabaki nayo hadi nitakapoenda kaburini.” Nuh aliiambia tovuti ya
Times Fm.
Hata
hivyo, Shilole alisema kuwa hatajichora kwa kuwa Nuh kafanya hivyo na
kwamba anashukuru kwa uamuzi wake kwa kuwa hakulazimishwa na ni ishara
ya upendo wa kweli tofauti na aliowahi kukutana nao awali.
“Siwezi
kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi tu na mimi siku
nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye. Kiukweli ana love
ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa nao, watu walikuwa
wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka kutafuta kick na
lakini Nuh kama Nuh ana upendo wa peke yake kabisa. Yaani hadi inafikia
hatua nasema alikuwa wapi. Wanasema Mungu akitaka kukupa kitu
hakuandikii barua.”

Uamuzi
wa Nuh Mziwanda unaendana na uamuzi alioufanya Nick Cannon na Mariah
Carey mwaka 2008 walipojichora tattoo za kudumu kwenye miili yao baada
ya kufunga ndoa. Nick aliandika mgongoni ‘Mariah’, na Mariah alijichora
kipepeo chini ya mgongo na kuandika maandishi madogo ‘Mrs Cannon’.
“Kwangu
mimi pete ni maalum na zinavutia, lakini tattoo zinamaana zaidi kitu
chochote. Ni za milele na milele…” Alisema Mariah Carey.
Lakini wamebaki na alama za tattoo kwenye maisha yao ambazo hazitafutika daima hata watakapokuwa na wapenzi wengine.
Hata hivyo, tattoo inaweza isiwe kitu kama watoto wao mapacha ambapo pia ni kiunganishi kikubwa katika maisha yao.
Tunawatakia kila la kheri
No comments:
Post a Comment