ALLY KIBA MSANI MWENYE VOCAL NZURI SOMA MACHACHE KUTOKA KWAKE
Ni
msanii ambae wengi sasa hivi wanapenda kusikia kutoka kwake sababu kwa
zaidi ya miaka mitatu aliyokua kimya, hakufanya interview na chombo
chochote cha habari wala kuonekana ovyo.
Baada yakurudi kwa kuachia nyimbo mbili mfululizo kwenye Radio, Ali Kiba ameanza kuchukua headlines bongoflevani.
23 August Ali amepiga show yake ya pili toka ukimya wa miaka mitatu ambayo ameipiga Tanga kwenye uwanja wa mpira uliokua umejaa maelfu ya watu kwenye tamasha la Fiesta.
Baada tu ya kuifanya hii show aliposhuka backstage, Ali alisema anashukuru Mungu watu wamempokea vizuri kuanzia show ya kwanza aliyoifanya uwanja wa taifa Dar es Salaam na kwamba video zake mbili zinaweza kutoka mwishoni mwa mwezi huu.
Anasema show yake ya mwisho kuifanya ilikua 2012 ambapo kwenye sentensi
nyingine Ali ameahidi huu ni mwendo wa kutopumzika yani, hatopumzika
tena kutoa nyimbo hivyo wimbo wake mwingine mpya anaweza kuutoa November
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment