Jarida la kimataifa la Euromoney la Uingereza limeitaja NMB kuwa
benki bora Zaidi kwa mwaka 2014 katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo
iliyofanyika jijini London hivi karibuni. Hii ni mara ya pili mfululizo
kwa NMB kutajwa kama benki bora Tanzania ambapo mwaka 2013 pia NMB
iliibuka kidedea na kutajwa benki bora Tanzania-2013.
Kila Mwaka, Jarida la Euromoney huandaa hafla ya kuyatambua Zaidi ya
Makundi 20 ya bidhaa za kitaasisi za kifedha zikiwemo benki kote duniani
kwa kuagalia benki bora na ya kiwango cha juu kwa kila bara na benki
bora katika nchi takribani 100 duniani kote. Tuzo hii huzitambua taasisi
za kifedha duniani kote ambazo zimepata mafanikio ya hali ya juu katika
maeneo yao, kwa kuonyesha ugunduzi na kupata mafanikio ya kifedha kila
mwaka.
Jopo la wataalam kutoka mataifa mbalimbali
na wenye utaalamu mbalimbali hupitia taarifa zinazowasilishwa na taasisi
zote za kifedha duniani na kutangaza washindi.
Ndani ya miezi 12, benki ya NMB imeanzisha huduma mbali mbali za
kibenki na hivyo kuendelea kuwafikia wateja wa huduma za kibenki kuanzia
kuweka akiba, kutoa na kuchukua fedha mijini na vijijini. Kama benki ya
kitanzania yenye wateja Zaidi ya milioni 2, Mpango wa NMB unadhihirisha
dhamira yake kuhusu elimu juu ya masuala ya kifedha kwa watanzania.”
Alisema Mark Wiessing.
“Tunatoa shukrani zetu wa wateja, wafanyakazi na washika dau wote kwa
kuwa sehemu ya mafanikio haya makubwa kwa benk, “ alisema Wiessing na
kuongeza kuwa NMB itaendelea na ahadi yake ya kuwapa huduma bora wateja
wake sasa na siku za mbeleni.
Wiessing aliongeza pia kuwa tuzo hiyo inaongeza kwenye hazina ya tuzo
ambazo benki imezipata katika miezi 12 huku akizitaja baadhi kuwa ni
benki bora ya mwaka kutoka jarida la Banker, Mamlaka ya mapato Tanzania
(TRA) wakiipa NMB tuzo ya mlipakodi anaefuata sharia katika taasisi za
kifedha nchini. Mwaka 2013 jarida la Euromoney pia liliitaja benki kuwa
Benki bora Tanzania huku taasisi ya Super Brand ya Kenya ikiitaja benki
bora Tanzania katika taasisi 20 bora Tanzania kwa 2013/3014 na Jarida la
the Banker pia liliitaja NMB kuwa benki bora ya kibiashara Afrika
Mashariki.
No comments:
Post a Comment