Mshambuliaji wa Man United Wayne Rooney ambaye hivi karibuni alipewa
cheo cha kuwa Nahodha wa timu yake wa Man United sasa amekabithiwa cheo
kingine kikubwa zaidi kwenye soka.
Baada ya Steven Gerrard kustaafu soka la kimataifa ,Rooney mwenye miaka
28 ameteuliwa kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na kocha wake
Roy Hodgson.Mpaka sasa Rooney amefunga magoli 40 kwenye mechi 95 na timu
yake ya taifa. Kwenye website yake Rooney ameandika “hii ni kazi
nitakayojituma kuifanya kuliko,na nimefurahia sana uteuzi huu, ni kama
ndoto kuwa kweli ”
No comments:
Post a Comment